KARI T A A R I F A
Toleo la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Kenya, Julai
1997. Nambari 1
Mtama wasaidia kutosheleza
akiba ya chakula nchini
Katika sehemu zenye uhaba wa mvua nchini Kenya, wengi wanantambua
mtama una nafasi bora zaidi kutosheleza akiba ya chakula.
Mtama ni mmea wa kiasili nchini Kenya.
Hata hivyo, ulipungua dhamana yake kwa wakulima kwenye
sehemu ambazo mahindi yalipendekezwa kuwa mmea na chakula
bora zaidi. Kwa wakati huu, wakulima wengi wanazidi kutambua
kuwa mtama ndio unaweza kufanya vizuri katika sehemu ambazo
mahindi yameshindwa kustawi.
Katika wilaya ya Machakos ambayo ilikumbwa na ukame mwaka
wa 1996, wakulima waliopanda mtama walipata mavuno mazuri
ikilinganishwa na mavuno ya wale waliopanda mahindi. Pius
Mwania na mke wake Jane wanatoa ushahidi wa tukio hili.
"Wale waliopanda mahindi hawakuvuna chochote",
alisema Bi. Mwania.
Wakiwa baadhi ya wakulima wengi wilayani Machakos, Bwana
na Bi. Mwania, hupenda mtama aina ya KARI/Mtama-1 ulioendelezwa
na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini Kenya - KARI. Mtama
huu ulitolewa mwaka wa 1994 na umevutia wakulima nchini;
wengi husema kuwa ni mtamu na unaweza kutumika kwa kupika
ugali wa ngano ili kuoka mikate na chapati. Aina ya mtama
uliyo na mbegu za rangi ya maji kunde unaojulikana kama
Seredo (na ambao pia uliendelezwa katika vituo vya utafiti
vya KARI, na hutumika kwa kupika ugali na uji. Kampuni maarufu
ya kuoka mikate, Makatiat Ltd., hushirikana na KARI kwa
utumiaji wa KARI/Mtama-1 kwa kuoka mikate (asili mia 15
ya unga wa mtama na 85 unga wa ngano), keki na biskuiti
(asili mia 50 unga wa mtama na 50 unga wa ngano).
Huko magharibi mwa Kenya na mkoa wa Nyanza, mtama hutumika
sana kama chakula cha kuku. Wakulima katika sehemu hii husema
kwamba kuku wa kienyeji hutaga sana wakilishwa mtama. Ugali
wa mtama hudhaminiwa sana katika sehemu hii haswa ukichanganywa
na unga wa mihogo.
Kufuatia ombi la viongozi katika wilaya ya Baringo wakitaka
usaidizi wa mimea ambayo huweza kustawi katika sehemu zinazokumbwa
na ukame mara kwa mara, KARI ilianzilisha mradi wa ujamaa
wa kiumarisha ukuzaji wa mtama huko Cheplambus, sehemu yenye
mabonde na milima. Ukosefu wa mvua katika sehemu hii husababisha
uharibifu wa mahindi kabla hayajakomaa.
Mtama aina ya KARI/Mtama-1 ulijaribiwa katika wilaya ya
Baringo ili kutosheleza akiba ya chakula na pia kama kielelezo
cha hali iliyoimarishwa katika mbinu za kutunza mimea na
kuzalisha mbegu zaidi. Mradi huu ulianzishwa mwaka wa 1992
na tangu wakati huo, eneo linalokuzwa mtama limepanuka na
mazao kwa wakulima yakaongezeka.
Mmoja wa wakulima wanaoshiriki kwennye mradi huu ni Bwana
Charles Rutto mwenye umri wa mika 38 na jamii ya watoto
6. Bwana Rutto amekuza mtama kwa miaka 5. Amepanda ekari
5 katika shamba lake na 5 katika shamba la kukodisha. Yeye
huamini kuwa sehemu hii ya Baringo imefaidika zaidi kutokana
na juhudi za mradi huu na hivi karibuni itajitosheleza kwa
chakula. Chakula cha mchanyiko wa mtama na maharagwe huliwa
na jamii nyingi na wameridhika kwamba ni chakula kitamu
kilicho maarufu.
Bwana Rutto na wakulima wengine wameanzisha chama ushirika
wa wakulima kitwacho EMKWEN Farmers Society kinacho wapatia
huduma za kupima uzito wa mtama, uhifadhi, ununuzi wa magunia
na uchukuzi.
Mkulima mwingine asili wa mtama ni Bwana Wilson Kipng'ok
anaetambuliwa kwa uhodari wa kutunza mtama. Shamba lake
limetumika kama uwanja wa kuonyesha na kuelezea wakulima
mbinu halisi za kutunza mashamba, kupanda mbegu, matumizi
ya mbolea, kupanda mtama na mbaazi kwa kutumia mbinu za
kilimo mseto na kupalilia. Bwana kipng'dk hutumia jembe
la kukokotwa na ng'ombe kuchimba mitaro ya kuhifadhi udongo
na maji shambani.
Ndege husababisha hasara kwa wakulima wa mtama katika
sehemu nyingi kwa wakulima wa mtama katikja sehemu nyingi
nchini. Njia moja inayotumiwa na wakulima kwa kufungwa kwenye
vikingi vilivyozunguka shamba. Mikebe hiyo huunganishwa
kwa kamba ambazo zikivutwa husababisha makelele yanyowafukuza
ndege
KARI imedhihirisha manufaa ya KARI/Mtama -1 kwa kuchanganya
na nafaka nyingine (k.m. wimbi wa kiasili, wimbi aina ya
Pearl na ngano) kwa kampuni zinazosaga unga nchini kama
KEN-UJI Products wilayani Meru na Elina ASAL Food Products
Wilayani Embu. Bw. Stephen Marete wa KEN-UJI hununua mtama
kwa wingi (gunia 500 na zaidi) kutoka kwa wakulima katika
wilaya ya Tharaka Nithi.
Vituo vya KARI huko Perkerra, Katumani, Kisii, Embu na
Kakamega vinashirikiana na vikundi vya wakulima vinavyokuza
mtama. KARI inanuia kuwapa wakulima wengi wanaoweza kunufaika
katika sehemu hizo mbegu na habari za ukuzaji wa KARI/Mtama-1
kupitia kwa vituo vyake vya utafiti. Mmea huu hufanya vizuri
katika sehemu zenye miinuko ya kati ya nita 50 hadi 1700
juu ya usawa wa bahari, na zenye mvua ya kiasi cha milimita
300 au zaidi. Sehemu zinazopendekezwa kwa ukuzaji wa KARI/Mtama-1
zinajumuisha mikoa ya Mashariki, Magharibi, Nyanza na Bonde
la Ufa (sehemu kama Baringo, Turkana, Pokot Magharibi, Nakuru)
na sehemu kadhaa katika mkoa wa Kaskazini Mashariki. KARI
imenunua mbegu kutoka kwa wakulima na kuzisambaza katika
vituo vya utafiti, kwa maafisa wa kilimo wilayani na kwa
vikundi vingine vinavyoweza kunufaishwa na KARI/Mtama
WIMBI WAJITOKEZA
Wimbi ni mmea ambao umekuzwa kwa muda mrefu barani Africa.
Wimbi una uwezo wa kustawi katika sehemu zenye uhaba wa
mvua ndiyo sababu umejumlishwa na mimea mingine ambayo inasaidia
kutosheleza akiba ya chakula nchini Kenya.
Umaarufu wa wimbi ulionekana wazi wakati wa misimu ya
kupanda ya mwaka wa 1996. Huko wilayani Kakamega, duka la
kuuzia mbegu la kampuni ya Kenya Seed Company liliuza mbegu
zaidi ya maradufu ya zile zilizouzwa mwaka wa 1995. Afisa
mmoja wa kampuni hii alisema kwamba wakulima wengi walinunua
mbegu za wimbi kwa sababu mapato ya mahindi ya mwaka uliopita
hayakuwa mazuri. Baadhi ya mbegu za wimbi ziliuziwa miradi
ya ukulima ya vijana na shule za upili.
Wanasayansi wa KARI wameutia wimbi maanani zaidi. Kituo
cha utafiti cha Kakamega kilianzisha mradi mkubwa wa kuzalisha
wimbi. Mradi huu tayari umefaidika kwa kupokea mbegu kutoka
sehemu mbali mbali nchini ambazo zinafanyiwa utafiti. Kutokana
na matokeoya uchunguzi wa mbegu hizi, KARI imetoa aina kadhaa
za mbegu za wimbi kama, P224 iliyo maarufu, na KAT/FM-1.
Wimbi hukomaa na kutoa mazao ya kuridhisha katika sehemu
ambazo mahindi hayastawi. Licha yakuwa wimbi haukuzwi kwa
wingi kama mtama, ni chakula chenye manufaa ambacho kina
madini muhimu kama calcium. Jamii za mapato ya juu zinazidi
kuzoe chakula cha wimbi na kuna majribio ya kujumlisha wimbi
kwenye baadhi ya vyakula vya watoto. Ugali na uji uliopikwa
na unga wa wimbi unazidi kuwa maarufu kote nchini. Juhudi
za kuvumbua kinga ya kuzuia wadudu na kwekwe wanaodhuru
wimbi na hata inzi wanaovamia mimea michanga zazidi kufanyiwa
uchunguzi katika kituo cha Kakamega. KARI imechapisha matokeo
ya mbinu za kisasa za upanzi, matumizi ya mbolea na ukuzaji
wa wimbi.
Watafiti wa KARI wanashugulika kuendeleza wimbi aina ya
Pearl ambao hukomaa mapema na hivyo kuepuka misimu ya ukame.
SHUKRANI
Taarifa hii inayoendeleza matokeo ya utafiti wa kilimo imedhaminiwa
na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Amerika (USAID) kwa
jukumu la Mradi wa KARI wa Utafiti wa Kilimo Nchini (NARP)
Editor: Dr. J. O. Mugah
Layout: Ms. Grace Kimani
Fore more info.
Director, KARI
P. O. Box 57811
Nairobi, Kenya
Tel. 254-02-583301-20
email: Director@kari.org
email: Resource.center@kari.org
|